Posts Tagged ‘ Starehe na kpub ’

EASTER HOLLS/PASAKA NDANI YA KP

Sikukuu ya Pasaka [Easter] Husherehekewa Ulimwenguni kote. Kama kawaida Kituo cha Starehe kwa Watu Makini cha Kiluvya Pub mambo kweli yalikuwa mambo. Burudani ya nguvu iliyoweka kumbukumbu Mioyoni mwa waliokuwepo ni ngumu kuisimulia.
Ngoja walao kwa Muhtasari tu uone kupitia Picha. Cha muhimu fanya hima na wewe kama hujawahi kufika Fika hasa siku za Week End nakuhakikishia utafurahia tuu. Karibu sana.

Studio ya Kiluvya Pub.

DJ Muddy. DJ mkali na hatari sana katika miondoko yote Bongo flava mpaka vitu vya mamtoni, akiwalusha Kiluvya Pub mpaka kuchee, Mablaza Men na Masista Duu wanamjua, Viti havikaliki. Jamaa mkali sana.

Ukishajiburudisha namna hii fikra na akili nazo zinatulizana unaporudi darasani kushika kitabu Material yanakubali kiulaini

Hapa kama sikosei nadhani wimbo uliokuwa unachezwa ni Kitambaa cheupe wa King Kikii. Si unaona huyo alivyonyanyua Kitambaa chake cheupe.

Sio lazima uende Dancing Floor. Hapohapo ulipo unaweza kuserebuka mpaka bas.

Heti mzee wa Macharanga Charles Hillary hebu niambie vipi Ile Thatched House ya kule East London inaona ndani kwa Kiluvya Pub?
Swali hilo pia ni kwa Brother Solomon Mugera pia Hassan Mhelella

Advertisements

WIDE SCREEN LIVE FOOTBALL

Hujutii  muda wako unapokuwepo Kiluvya Pub kwani ni mahali ambapo mbali na Burudani kadhaa utajionea Michezo ya Ligi mbalimbali za Barani Ulaya na Afrika pia Mashindano ya Champions League. Huonyeshwa kupitia Screen kubwa kama inavyoonekana hapo. Mashindano ya Kombe la Dunia Yataonyeshwa pia kaa mkao wa kula.

Kiluvya Pub ni Mahali ambako Ligi mbalimbali Barani Ulaya pia Champions League zinaonyeshwa kupiti Screen kubwa kama inavyoonekana hapo katika mpambano baina ya Bayern Munich Vs. Man United

Wapenzi wa Football wanafuatilia Mpambano.

EASTER EASTER EASTER – PASAKA PASAKA PASAKA

EASTER EASTER EASTER – PASAKA PASAKA PASAKA
Usikose uhondo ndani ya Kituo chako cha starehe Kiluvya Pub,
Muziki mkali na Djs waliobobea kutoka Kiluvya Djs Group na Nje ya Pub. Fanya Pasaka yako iwe safi na Kiluvya Pub.

YALIYOJIRI SIKU YA VALENTINES DAY NDANI YA KILUVYA PUB 2010

Binti huyo ndie aliyepata ushindi wa Mnenguaji bora kwa siku hiyo ya Valentine Day. Amepata tuzo ya kitenge cha Wax. hapo anaonesha umahiri wake

Kijana huyo ndie alieonekana na Majaji kuwa ndiye mnenguaji hodari. Hapo anaelekea Dancing Floor kuonesha umahiri wake baada kutangazwa kuwa mshindi kwa upande wa Wanaume. Amepata Zawadi ya Shati zuri sana.

Mshindi wa Valentine Day akionesha na kufurahia zawadi yake ya Simu {Nokia}

Judge akimtangaza mshindi alievaa Ki-Valentine Day ambapo alizawadiwa Simu aina ya NOKIA.

Chief Judge akitangaza Washindi na kueleza vigezo vilivyoyumika kuwapata Washindi hao. Walipatikana wanenguaji hodari wa Kike na Wakiume pia alievaa vizuri Ki-Valentine

Mkuu wa Kitengo cha Itifaki Bwana Lukindo akionesha umahiri katika kucheza Muzidi.

Wahudumu wa Kiluvya Pub wakiwa na Meneja wao Bi. Angel Sanga [Kulia]

Ndani ya Kiluvya Pub Watu wa marika yote wanapata Burudani isiyo kifani inayoporomoshwa na Ma Dj makini kwa Mashine za hali ya Juu. Hupotezi muda wako unapofika Pub. Usingoje kusoma ama kuhadithiwa. Fika mwenyewe uburudike.

Sherehe Ndani ya Ukumbi wa Kiluvya Pub siku ya Wapendanao [Valentine Day]. Wahudumu wakiwa Tayari kutoa Huduma safi isiyo na kasoro ya aina yoyote. Siku hiyo ilikuwa murua sana. Wote waliokuwepo wamesema hawataisahau kwa jinsi walivyostareheka kwa namna mbalimbali.

Vitu vikali ndani ya Pub, Kiluvya Pub Bwana, Wee Acha tuu

Nahisi Wadau Bakari Msulwa huko Tokyo Japan, Joe Nyingo huko Washington DC, Ismail Misigalo huko Kigali Rwanda, Lubunga Biaombe, huko Kinshasa na hata Chekuse Kawawa huko Dublin , Ireland. Mnai Miss Kiluvya Pub!! Au?

BLU 3 feat. MOSES – WHERE YOU ARE, VALENTINES DAY 2010

VALENTINES GIFT!!!!!!!!!!! Fine future tune itafanya Valentine yako iwe swafi, maandalizi makali ndani ya Tarehe 14 Feb hii Djs wakali watafanya Valentine iwe siku ya ndoto kamilifu kati yako na mwenza wako, Usizubae jiandae kuifurahia siku hii muhimu kwa wapendanao ndani ya Kiluvya Pub. Red Roses and white and Red Dress zitatawala na zawadi zitatolewa kwa washindi wa vazi la Valentine. Check it Out in our contacts (About Us) for more details and any doubts

Vodpod videos no longer available.

 

HAPPY NEW YEAR 2010

London mpaka Bongo

Mdau Israel Saria ndani ya Kiluvya Pub, Safari yake toka jijini London aishipo mpaka Tanzania kwa mapumziko ya muda mfupi. Karibu tena Kiluvya Pub Mambo haya yote ni kwa hisani kubwa ya wadau wote wa Kiluvya pub. Bwana Saria anapatikana katika Blog yake maarufu inayorusha mambo yote na taarifa zote muhimu katika suala zima la michezo Spoti, bonyeza hapa ujionee mwenyewe, tanzaniaspots

Mdau wa Kiluvya Pub, Bw Israel Saria, akimlisha keki kijana wake Gerson katika sherehe za kipa imara, jijini Dar Hivi Karibuni.

Advertisements