Posts Tagged ‘ KiluvyaPub Pichani ’

Mamboz katika kituo chako cha starehe.

Kanisa Lako Kiluvya

Ndugu zangu, mnakumbuka niliwapeni Taarifa mapema kuhusu Harambee tunayotarajia kuifanya mwezi wa ujao wa June. Nawakumbusheni kuwa Kanisa hilo linajengwa kwa Nguvu za Waaamini wa Kigango cha Kanisa Katoliki la Kiluvya. Wameanza tangu Msingi hadi kufikia hali hiyo. Ingawa linaonekana hivyo lakini bado halijakamilika. Tupo katika Final Touches. Tarehe 28 June,2009 tutakuwa na Harambee hapo Kanisani kwa ajili hiyo.Nawaombeni wote wenye Mapenzi Mema mtuunge Mkono. Mimi ndie Mwenyekiti wa Ujenzi. Niungeni Mkono mwenzenu Jamani. “Mwenye ukarimu atabarikiwa na Bwana”(Mith 22:9) “Abishae hodi atafunguliwa” (Luk 11:10);” Mtu mwema atamthamini mwenzake” (Yob 29:14) Unaona nilivyochimbua hapo hivi kweli mtaniacha hivihivi.

Kanisa Katoliki Kiluvya

Recreation involves sport
Eeh, kazi kubwa. Mashindano ya kuvutana kwa kamba katika ya Sherehe za Somo wa Parokia ya John Bosco Tumbi, Kibaha.

Mashindani akina mama wa Kiluvya
Eeh, kazi kubwa. Mashindano ya kuvutana kwa kamba katika ya Sherehe za Somo wa Parokia ya John Bosco Tumbi, Kibaha.

Taifa la kesho - Matombo

Watoto wanapocheza Twist.! Lakini haikuchezwa ndani Pub.

Masela nao wamo

Wacha bwana jamaa Muziki umewakolea kisawasawa. Si unawaona

Matukio mbalimbali

Kiluvya Pub huwa inapambwa kwa Stahili tofauti kutegemea na Matukio

Champagne

Shampeni hufunguliwa wakati wa Matukio Muhimu

Wadau (fans) wa Kiluvya Pub
Yaani ni Furaha tupu Pub. Ukitaka uelekezwe Kiluvya Pub ilipo usipate shida wewe sema tu Pub iko wapi hata mtoto Mdogo atakuonesha. Ona jamaa wanavyofurahia. Yaani Muziki wa hapo ni vigumu sana kuupata sehemu nyingine ya Dar. Kama huamini fika mwenyewe ukajionee.

Yero ndani ya Pub

Pub ni Sehemu inayopendwa na kila Mtu. Si unamuon jamaa huyu wa Kimasai nae kafika kujiburudisha

KILUDEA
Kiluvya Ni Kijiji kilichokuwa kwa haraka sana. Hivi sasa kimpata Hadhi ya kuwa Mtaa. Wana Kiluvya wameunda Umoja wao unaojulikana kama Kiluvya Development Association (KILUDEA) Ni Asasi ya kijamii isiyo ya Kiserikali (NGO) Madhumuni yake ni kusukuma maendeleo ya Eneo lao ili kupafanya pawe mahali pazuri pa kuishi. Tarehe 19April 2009 KILUDEA waliomba kuzungumza na Waziri wa Ardhi na Makazi afike Kiluvya wazungumze naye kuhusu Mpango unaofikiriwa kutekelezwa na Wizara yake kupuma na kuboresha mazingira ya Mtaa huo. Wana KILUDEA walitaka Wana Kiluvya kama Wadau washirikishwe katika kutekeleza Mpango huo. Hapo Mwenyekiti wa KILUDEA anafungua kikao hicho. Waziri alishindwa kufika kwa Udhuru lakini alituma Maofisa wake wa Mipango Miji kumuwakilisha.

KILUDEA

Sehemu ya Wanachama wa KILUDEA wakimsikiliza Mwenyekiti wao

Maofisa Wizara ya Ardhi

Maofisa kutoka Wizara ya Ardhi na Makazi waliotumwa na Waziri wa Ardhi kuja Kiluvya kozungumza na Wanachama wa KILUDEA . Hapo wonge.anamsikiliza Mwenyekiti wa KILUDEA akiwapa vid

Advocate Safari

Engineer Charles Mvungi Mwana Kiludea ana Mji wake Kiluvya. lakini kwa sasa anaishi na kufanya kazi zake huko Johannesburg, South Africa kama Mhandisi. Siku ya kikao hicho muhimu alikuwepo kama anvyoonekana akitoa Ushauri kwa Maofisa wa Ardhi

Engineer Charles Mvungi

Wahudumu wa KPub
Wahudumu wa Kiluvya Pub wanapokuwa katika maandalizi ya kuhudumia.

Mkurugenzi na Charles Hillary
Mkurugenzi wa Idhaa ya Kiswahili a BBC , London Bwana Solomon Mugera ananena jambo na Mwenyekiti.

PROTOCALS
Mkurugenzi wa Idhaa ya Kiswahili a BBC , London Bwana Solomon Mugera ananena jambo na Mwenyekiti.

Wadau wa Kiluvya Pub
Mzee wa Blog ya Jamii Bwana Issa Michuzi naye alifanya nia kuitembelea Kiluvya Pub. Muulize atakusimulia aliyoyaona.

Waheshimiwa Charles Hillary na Issa Michuzi
Mzee wa Blog ya Jamii Bwana Issa Michuzi naye alifanya nia kuitembelea Kiluvya Pub. Muulize atakusimulia aliyoyaona.

Mkurugenzi idhaa ya kiswahili BBC

Habari za Kiluvya Pub na Sifa zake zimewafikia watu wengi Duniani kote. Hata Waishio Uingereza Sifa hizo zimekwishawafikia. Mkurugenzi wa Idhaa ya Kiswahili,ya BBC, London naye amtinga ndani ya Kiluvya Pub. Hapo anaelezea jinsi alivyofurahi kufika mahali hapo. Amewahi kusimuliwa na Vijana wake kama Lubunga Byaombe wa DRC, Ismail Misigalo wa Burundi na wengine wengi waliowahi kufika. Ameshangaa kuona mahali pazuri penye Burudani ya nguvu ikiwa Nje ya Jiji. Ameahidi kuitembelea tena. Je wewe vipi? usipitwe. Tembelea Kiluvya Pub Week EndUjiburudishe baada ya kazi zako.

Timu nzima ya BBC Swahili.

Bwana Solomon Mugera, Boss (Mkurugenzi) wa Idhaa ya Kiswahili BBC, London naye ameshindwa kukaa kitini amejikita Ndani ya Dancing Floor kujiburudisha . Muziki anaokwenda nao ni ule wa Embakasi uliopigwa na Less Mangelepa.
Mambo haya yote ni kwa hisani kubwa ya wadau wote wa Kiluvya pub.

Kula ngoma, si mchezo.

Fans wa kiluvya Pub
Wimbo ukikupendeza sharti uuimbe kama anavyoonekana Mzee wa Macharanga anashika Moyo kufuatilia Wimbo wa Msondo ndani ya Kiluvya Pub.

Charles Hillary ndani ya kiluvya Pub
Wimbo ukikupendeza sharti uuimbe kama anavyoonekana Mzee wa Macharanga anashika Moyo kufuatilia Wimbo wa Msondo ndani ya Kiluvya Pub.

Mzee wa macharanga Charles Hillary.
Mzee wa Macharanga Bwana Charles Hillary, baada ya kazi kubwa ya mafanikio ya kuwakutanisha watoto wa Marais wa zamani wa Tanzania na Uganda huko Butiama hapo anajibudisha na Muzikiwa Msindo

MKURUGENZI SOLOMON MGERA

MKURUGENZI SOLOMON MGERA
Burudani ndani ya Kiluvya Pub, Wee acha tuu.  Kama hujawahi kufika basi tia hamu nawe ufike. Hutajutia muda wako.

MKURUGENZI SOLOMON MGERA

Mduara huo, mambo yamekuwa mambo.

Advertisements
Advertisements