Posts Tagged ‘ Kiluvya pub ’

Kiluvya Pub mpaka London.

 

Mr Luanda BBC London
Mwenyekiti kutokana na kufahamika kwake kuwa ni Mwanamichezo, hapo amepewa nafasi kutoa Uchambuzi alivyouona Mchezo kati ya Liverpool V Hull City. Hapo ni ndani ya Studio za BBC, Bush House, London. Anaemsikiliza ni Mchambuzi maarufu Bwana Israel Saria na kulia kwa Mwenyekiti ni Mtangazaji wa BBC Bwana Peter Musembi.

Chelse fan Mr Luanda
Hapa sikuwa na Ujanja. Nilijibatiza kuwa Mpenzi wa Chelsea kwa muda. Tiketi niliyokata ni kukaa Eneo la Mashabiki wenyeji Chelsea. Bendera unaikuta kwenye Kiti. sasa utafanyaje.

Chelse Vs Barcelona

Tarehe 7/5/2009 Jumatano, Nusu Fainali ya Pili Mashindano ya Mabingwa Kombe la Ulaya 2009 Kati ya Chelsea V Barcelona . Mpambano huu uliochezwa Stamford Bridge Uwanjani Kwa Chelsea Football Club, ni wa Marudiano baada ya ule uliochezw Nou Camp huko Barcelona. Hapo Timu nfio zinakaguliwa. Ndoto ya Chelsea kucheza Fainali ili walipe kisasi cha kufungwa na Man U mwaka jana kwa Mikwaju ya Penalt, leo yameyeyuka baada ya kulazimishwa sare ya 1-1.

Nusu fainali kombe la ulaya 2009

Mpambano mkali kila Mchezaji yupo makini

askari Usalama
Askari wa Farasi wapo kazini Kudhibiti Usalama

Chelse Stadium
Stadium la Chelsea linavyoonekana kwa mbele.

Barcelona fans
Mashabiki wa Barcelona wakiwa katika Picha ya pamoja kabla ya Mpambano hapo Stamford Bridge.

UEFA LOGO
Tambaa kubwa ambalo linabeba Nembo ya UEFA kama linavyoonekana Uwanjani Stamford Bridge.

Arsenal Vs Man United
Siku Arsenal ilipotolewa Nishai na Wapinzani wao wa Jadi Manchester United kwa kufungwa magoli 3-1. Screen kubwa iliyopo Uwanjani Emirates ilisomeka hivyo kabla ya Mpambano.

Emirates Stadium
Usiku wa leo Tarehe 5/04/2009 ni mgumu sana kwa sie Wapenzi wa Arsenal. Mchezo wa Nusu Fainali ya UEFA Champions League umechezwa Emirates Stadium. Na mimi niliingia Uwanjani kama wenzangu tukiwa tumejiamini sana kuwa tungewaondosha Man U. Viti vyote viliwekwa bendera zisaidie kushangilia. niliinyanyua bendera yangu kwa kujiamini! Loo, mambo hayakuwa mambo tumetoka Uwanjani tumelowa.

Soko dogo London-african food

Advertisements
Advertisements