NAUMIA ROHO – DULLAYO

Kiwango cha muziki wa kisasa bongo kipo juu sana baadhi tu ya wasanii wadogo mambo wanayofanya ya kiwango cha kimataifa. Dullayo ni mmoja kati ya vizazi vipya ambaye kwa kiasi kikubwa kila kitu atoacho kinakonga nyoho nyingi za wasikilizaji ndani na nje ya nchi. Hongera Dullayo unakaribishwa kupata kinywaji Kiluvya Pub, pia kutoa burudani kwa wapenzi wa pub.

Vodpod videos no longer available.

more about “NAUMIA ROHO – DULLAYO“, posted with vodpod

 

Advertisements

Dully Sykes – Shikide na KP DJs

Vodpod videos no longer available.

more about “untitled“, posted with vodpod

 

Kiluvya Pub inawajali watoto pia.

Kituo cha Burudani cha Kiluvya Pub kinawajali watu wa Marika yote. Kwa siku za Sikukuu kama ya Eid El Fitr, Christmas na nyinginezo, watoto wanaandaliwa muda maalum peke yao kuburudishwa. Hapo wanaonekana watoto wakifurahia Muziki wa kizazi kipya unaoporomoshwa na Ma DJ waliojipanga kutoka Mashine za hali ya juu. nakuhakikishia hupotezi muda unapokuwa Kiluvya Pub. Fanya hima uje ujiburudishe usingoje kuhadithiwa.

Kiluvya Pub

Ma DJ. wa Kiluvya Pub, kutoka kusoto DJ Scope V. na DJ Muddy wakiwa katika kurekebisha mashine tayari kuburudisha watoto.

DjS Mixing

Hawa jamaa wanafuatilia Mpambano wa Mechi baina ya Man U Vs. Man City
Huwezi kujutia muda wako unapokuwa ndani ya Ukumbi wa Kiluvya Pub kwani mbali na Burudani kunaoneshwa Mechi mbalimbali za Ulaya na pia Mashindano ya Champions League katika Screen kubwa. Ukipenda ita Pull Down Screen!

Wide-screen
Happy Birthday Mama.

Kiluvya Pub pamoja na uongozi mzima, tunapenda kumpongeza mama yetu mpendwa katika sherehe yake ya kuzaliwa. Bibie Shirley na mama yake wakiwa na furaha siku hiyo muhimu ndani ya mji wa Zwolle, inchini Netherlands. Mama pamoja na mwanawe Bibie Shirley wameahidi kuitembelea Kiluvya Pub mwakani katika safari yao inchini Tanzania katika jiji la Morogoro (Mji kasoro bahari) ambapo ndipo palikuwa makazi ya mama enzi hizo.
Tunakutakia sherehe njema, HAPPY BIRTHDAY MUM

Happy Birthday Mama

Mama na Mwana inchini Netherlands.

Bibie Shirley alipomtoa mama yake OUT kumpongeza kwenye Birthday yake, naona yupo kwenye pose.

Shirley - Happy Bday Mum

ManDojo And Domokaya Feat Maunda Zorro – Utanisimanga

ManDojo And Domokaya Feat Maunda Zorro – Utanisimanga. Vijana hawa wanastahili pongezi kubwa kwa style yao safi na kamilifu. Kiluvya Pub inawapa pongezi na Mungu azidi kuwapa upeo zaidi wa kuelimisha jamii hii ya Tanzania, pia kuiburudisha

Vodpod videos no longer available.

more about “ManDojo And Domokaya Feat Maunda Zorr…“, posted with vodpod

 

 

Harambee Kanisa La Kiluvya

Harambee - kiluvya pub

Tarehe 28/6/2009 Ilikuwa Siku kubwa sana kwa Waamini Wa Kanisa Katoliki Kigango (Sub Parish) cha Kiluvya. Ni siku ambayo nilieleza kuwa ingefanyika Harambee ya kuchangia Pesa za kumalizia Ujenzi wa Kanisa hilo. Harambee imefanyika kwa mafanikio makubwa ambapo kiasi cha Shilingi Milioni Milioni39,567,000/= zilichangwa ambazo Cash zilichangwa Shilingi 37,875,000/=. Marafiki zangu wote mlioahidi kuchangia bado nafasi ipo ya kuchangia.

Monsignor Julian Kangalawe-Askofu katoliki Tanzania

Monsignor Julian Kangarawe ambaye ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ndiye aliongoza ibada kwa siku hiyo ya Harambee.

Baba paroko

Baba paroko Fr. Alister Makubi akiwaandaa Waamini tayari kwa Harambee.

Mwenyekiti wa Kigango mama Hilda Banda akitoa Nasaha na kuzindua Harambee. Pembeni yake ni Msheheneshaji katika Harambee hiyo Ndugu Joseph Mmbando kutoka Jumuiya ya Mtakatifu Augustino

Mwenyekiti wa Ujenzi Bw. R.Luanda

Mwenyekiti wa Ujenzi Ndugu R. Luanda akitoa Nasaha katika Harambee hiyo.

Mwenyekiti wa Jumuiya iliyoshinda ya Mtakatifu Rafael Mama Rose Mbilinyi akikabidhi mchango wao wa Shilingi Milioni 11, Laki 1 na Sitini na Saba Elfu. Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi Ndugu R. Luanda yupo katika Jumuiya hii.

Wasanii mashughuli wa filamu za kibongo wakiwa Kiluvya Pub

DSC00788Kiluvya PubWasanii mbalimbali mashughuli wa filamu za kibongo zivumazo katika jiji la Dar-Es-salama, walitia timu ndani ya kiluvya Pub kujionea wenyewe jinsi gani Pub hiyo ilivyomvuto, na huduma pekee ambazo si kila Pub unaweza kuzipata. Walipokelewa vizuri na vitumbuizo kibao viliandaliwa kuwaalika ikiambatana na kumtafuta mlimbwende wa Pub hiyo, Djs wakiwa makini na muziki mdundo ulikuwepo. Wasanii waliokuwepo ni pamoja na Steven Kanumba, Vincet Kigosy (Ray), Blandina Chagulla (Johari), Mwanaidi Suka, Bonta, pamoja na wengineo wengi. Ni siku kubwa ambapo mastaa hao pia waliweza kutoa vitumbuizo na midodoso ya vitu kibao ili mradi kukamilisha lengo halisi yaani Starehe kwa watu Makini

Steven Kanumba -Kiluvya Pub

Blandina Chagulla-Kiluvya Pub

Bongocelebs

Je nanyi lini mtafika katika kituo cha starehe, muziki mkali na vinywaji vya kila aina vya kumwaga, yani mambo mzuka, tunawakaribisha sana Kiluvya Pub.

Advertisements