HAPPY NEW YEAR 2010

Advertisements

Msiba mkubwa Kiluvya

Kijijini Kiluvya hivi karibuni kwa mara nyingine Tumepatwa na Msiba Mkubwa wa kuondokewa na Bibi yetu Mpendwa Bibi Martha Moto.  Wanakijiji wote wa Kiluvya kwa huzuni kubwa walikusanyika nyumbani kwa Mkurugenzi wa Kiluvya Pub na Mwenyekiti wa KILUDEA Bw. R. Luanda kumpa pole kutokana na kuondokewa na mama yake mzazi Binti Moto ambaye alifariki wiki iliyopita nyumbani na hatimaye mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya tumbi.  Mazishi yamefanyika wiki hii kijijini Matombo ambako marehemu (Bibi) anatokea.  Wote tunampenda sana bibi yetu mpendwa LAKINI Mungu anampenda zaidi, ndugu jamaa na marafiki pamoja na wadau wote wa Kiluvya na sehemu yoyote duniani wanapenda kutoa POLE kwa familia nzima ya Bw. R. Luanda, Mwenyezi Mungu aiweke Roho ya bibi yetu mpendwa mahali pema peponi, Amen.

Bwana Robert Shrier kutoka Uingereza akimsalimia bibi siku chache kabla ya kifo.

Mheshimiwa Baba Askofu Methodius Kilaini akimsalimia Marehemu siku chache kabla ya umauti.

London mpaka Bongo

Mdau Israel Saria ndani ya Kiluvya Pub, Safari yake toka jijini London aishipo mpaka Tanzania kwa mapumziko ya muda mfupi. Karibu tena Kiluvya Pub Mambo haya yote ni kwa hisani kubwa ya wadau wote wa Kiluvya pub. Bwana Saria anapatikana katika Blog yake maarufu inayorusha mambo yote na taarifa zote muhimu katika suala zima la michezo Spoti, bonyeza hapa ujionee mwenyewe, tanzaniaspots

Mdau wa Kiluvya Pub, Bw Israel Saria, akimlisha keki kijana wake Gerson katika sherehe za kipa imara, jijini Dar Hivi Karibuni.

Furaha na Kiluvya pub

Mtangazaji Gwiji wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, London na Mpenzi mkubwa wa Kiluvya Pub Bwana Charles Hillary siku alipoadhimisha Siku yake ya kuzaliwa nyumbani kwake London. kulia kwake ni Binti yake Bi Faith Charles.

Duh! Kumbe Mdau Charles Hillary alikuwa na Mapooz tangu akiwa mdogo. Hapo alikuwa na umri wa miaka Minne.

Mwenyekiti wa Kiluvya Pub Akigongesha Glass na Bwana Charles Hillary kumpongeza katika Adhimisho la siku yake ya kuzaliwa.

Bi Martha Constantine Kalipeni (Kibe) Tarehe 27/10/2009 alihitimu Shahada yake ya ACCA huko London, UK. Pichani anaonekana akijiandaa kupewa Mkono wa pongezi na President wa ACCA Bwana Brendan Murtagh katika sherehe iliyofanyika Ukumbi wa Barbican Centre Jijini London.

Hongera sana Bi Martha.

Martha akibadilishana mawazo na Wahitimu wenzake.

Kumbe hata London vipo Vibajaji.

Kibajaji - London

Msiba mkubwa kijijini Kiluvya

Kijijini Kiluvya hivi karibuni kwa mara nyingine Tumepatwa na Msiba Mkubwa wa kuondokewa na Mama yetu Mpendwa Mama Katherine Saguti aliefariki na kuzikwa Kiluvya mwanzoni Octoba. Mama Saguti alikuwa Mwanachama mwanzilishi wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Kiluvya Development Assiciation ambapo alikuwa pia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Asasi hiyo. Mwenyezi Mungu aiweke Roho ya mama yetu mahali pema peponi, Amen.

Sanduku lililobeba Mwili wa Mama Katherine Saguti likiandaliwa kushushwa Kaburini

Mzee Lawrence Saguti Mume wa Marehemu Mama Katherine Saguti akiwa katika majonzi makubwa.

Mzee Lawrence Saguti wa pili kutoka kushoto


Katibu Mkuu Kiongozi Mheshimiwa Philemon Luhanjo alikuwepo katika Mazishi hayo.


Mwenyekiti wa KILUDEA akiweka Shada la Maua katika Kaburi la Mwanachama wake.

Mafahali Hondogo shule ya msingi

Wanafunzi waliohitimu Elimu ya Msingi 2009 Shule ya Kiluvya Hondogo wakiwa katika Picha ya pamoja wakionesha Vyeti vyao.

Kiluvya P/R School

Wanafunzi wa Darasa la kwanza Shule ya Msingi Hondogo, Kiluvya wakiimba Utenzi katika Mahafali ya Shule hiyo

Watoto wakiwaimbia wenzao nyimbo za kuwaaga katika Mahafali hiyo. Je unakumbuka enzi zako? nani hakupitia hayo?

Watoto wa Shule ya Msingi ya Hondogo wakiburudisha kwa kucheza Ngoma za Asili.

Ngoma za asili

Tanzania yetu

Bandari Salama napo Si Mchezo inaonekana poa pichani pia ni bandari mojawapo pekee kwa mizigo iingiayo inchini hata nchi jirani, ni sehemu moja kubwa kiuchumi inchini.

Bandari Salama

Mlima Meru, si mlima mkubwa sana ukilinganisha na Kilimanjaro lakini ni fahari kubwa pia ya Tanzania kwa watalii wafikao Arusha huufurahia.

Mlima Meru

 

 

Advertisements