About Us


Kiluvya Pub Kituo Cha Starehe Kwa Watu Makini.

KILUVYA PUB

Kiluvya Pub ilianzishwa mnamo mwaka 1997 ikiwa Pabu pekee katika eneo la Kiluvya lijulikanalo kama kijiji cha Kiluvya jijini Dar-Es-Salaam wilaya ya Kinondoni. Kijiji cha Kiluvya kipo nje kidogo ya jiji la Dar-Es-salaam barabara ya Morogoro, kipo karibu kabisa na Mkoa wa Pwani na baadhi ya huduma za kijamii wanakijiji wa Kiluvya hupata kutoka mkoa huo.

Lengo kubwa la Kiluvya Pub ni Mapumziko, Burudani, Maendeleo, Starehe na kujenga urafiki  kwa watu wote bila ubaguzi wa aina yoyote ile. Ni sehemu ambayo imetulia kuwakutanisha watu mbalimbali kutoka maeneo tofauti nchini na hata nje ya inchi. Huduma zetu ni za kiwango cha kuridhisha kukidhi mahitaji ya walengwa.

Pub hii ni sehemu tu ambayo kwa nafasi kubwa sana imeendeleza kijiji cha Kiluvya kujulikana Tanzania na hata duniani pia. Lengo ni kuipanua kimajengo na hata kuweka Lodge kwa ajili ya wale watokao nje ya nchi na labda wangependa kupunzika kwa siku kadhaa.

Mkurugenzi wa Kiluvya Pub ni mpenda maendeleo mkubwa katika nyanja mbalimbali za kiburudani hivyo kwa ukaribu kabisa mawazo mengi yanafikiriwa kuipanua na kuboresha zaidi huduma za pub yako uipendayo.

Hapa huduma zifuatazo zinapatikana, vinywaji vya aina zote (liquor and soft drinks), Chakula (Nyama choma), Muziki mkali Djs Mixing (Old School and current hits), Matamasha ya pub (Khanga party, Miss Kiluvya Pub, Miss Pwani events). Sherehe mbalimbali zinafanyika ndani ya Kiluvya Pub, unaweza kutoa bukingi ya kufanya sherehe yako yoyote hapa na pub itaku-accommodate na Muziki na baadhi ya huduma ambazo ziko nje ya uwezo wako.

Sherehe ambazo zinafanyika kwa wingi hapa ni pamoja na Harusi, Wahitimu chuo kikuu, kukaribisha wageni toka nje ya inchi, komunio, kitchen party, khanga party, Disco Dance.

Hivyo lengo la kuwakutanisha watu na kupata kile roho inapenda litakamilishwa kwa haraka zaidi na Kiluvya Pub. Tunapenda maoni jinsi ya kuiboresha zaidi na tunalipa kipaumbele kila oni lako juu ya kuiboresha Kiluvya pub.

Suala la ulinzi halina tatizo kwa wale wenye usafiri na ambao wanapenda starehe bila fujo, kuna walinzi walioandaliwa na pia polisi wanakuwepo kuweka ulinzi kwenye matamasha maalum na kituo cha Polisi kipo hapahapa jirani.

Kiluvya Pub Kituo Cha Starehe Kwa watu Makini:

 Katibuni Kiluvya Pub, Welcome to Kiluvya Pub, Karibuni sana Kiluvya Pub.

CONTACTS

Address

KILUVYA PUB,

P.O Box 33177

DAR-ES-SALAAM

TANZANIA

E-Mail Us.

kiluvyapub@gmail.com

kiluvyapub@yahoo.com

Phone No.

  0754305458 (Tanzania)

 Mkurugenzi Kiluvya Pub
 
Bw. Robert Luanda
 
 
 
 
 
 

 

Advertisements
Comments are closed.
Advertisements
%d bloggers like this: