Archive for April, 2010

MAISHA INJE YA BONGO NA KP

Kila kona ya mitaa ya Uingereza katika majiji yote na vitown vidogo kuna bar au Pub, Mitaa imepangiliwa na mtiririko wa nyumba kufuatana, pia mitaa iko safi na mazingira yamepangiliwa pamoja na ujenzi.
Hapo wanafunzi wa chekechea wakitoka shule na wasimamizi wao wakielekea majumbani kwao wakiwa na Hi-vest kwa ajili ya usalama barabarani.

Menus za baa na pabs kama inavyoonekana ratiba ya yaliyomo kwa wiki-end au siku za juma katika pab husika ndani ya Normanton Road Derbyshire Uingereza.

Kituo kidogo cha mabasi (Local transport), hapo sawa na kusubiri basi kutoka Africa-sana kuelekea Kariakoo au Posta Bongo, hapa ni Uingereza nje ya Jiji la London.

Hapa ni Uholanzi, Mitaa yake haitofautiani na Uingereza na ujenzi ukiangalia kwa makini unafanana, Bibi Shirley akiwa na rafiki yake, wabongo waishio Uholanzi.

Advertisements

EASTER HOLLS/PASAKA NDANI YA KP

Sikukuu ya Pasaka [Easter] Husherehekewa Ulimwenguni kote. Kama kawaida Kituo cha Starehe kwa Watu Makini cha Kiluvya Pub mambo kweli yalikuwa mambo. Burudani ya nguvu iliyoweka kumbukumbu Mioyoni mwa waliokuwepo ni ngumu kuisimulia.
Ngoja walao kwa Muhtasari tu uone kupitia Picha. Cha muhimu fanya hima na wewe kama hujawahi kufika Fika hasa siku za Week End nakuhakikishia utafurahia tuu. Karibu sana.

Studio ya Kiluvya Pub.

DJ Muddy. DJ mkali na hatari sana katika miondoko yote Bongo flava mpaka vitu vya mamtoni, akiwalusha Kiluvya Pub mpaka kuchee, Mablaza Men na Masista Duu wanamjua, Viti havikaliki. Jamaa mkali sana.

Ukishajiburudisha namna hii fikra na akili nazo zinatulizana unaporudi darasani kushika kitabu Material yanakubali kiulaini

Hapa kama sikosei nadhani wimbo uliokuwa unachezwa ni Kitambaa cheupe wa King Kikii. Si unaona huyo alivyonyanyua Kitambaa chake cheupe.

Sio lazima uende Dancing Floor. Hapohapo ulipo unaweza kuserebuka mpaka bas.

Heti mzee wa Macharanga Charles Hillary hebu niambie vipi Ile Thatched House ya kule East London inaona ndani kwa Kiluvya Pub?
Swali hilo pia ni kwa Brother Solomon Mugera pia Hassan Mhelella

WIDE SCREEN LIVE FOOTBALL

Hujutii  muda wako unapokuwepo Kiluvya Pub kwani ni mahali ambapo mbali na Burudani kadhaa utajionea Michezo ya Ligi mbalimbali za Barani Ulaya na Afrika pia Mashindano ya Champions League. Huonyeshwa kupitia Screen kubwa kama inavyoonekana hapo. Mashindano ya Kombe la Dunia Yataonyeshwa pia kaa mkao wa kula.

Kiluvya Pub ni Mahali ambako Ligi mbalimbali Barani Ulaya pia Champions League zinaonyeshwa kupiti Screen kubwa kama inavyoonekana hapo katika mpambano baina ya Bayern Munich Vs. Man United

Wapenzi wa Football wanafuatilia Mpambano.

EASTER EASTER EASTER – PASAKA PASAKA PASAKA

EASTER EASTER EASTER – PASAKA PASAKA PASAKA
Usikose uhondo ndani ya Kituo chako cha starehe Kiluvya Pub,
Muziki mkali na Djs waliobobea kutoka Kiluvya Djs Group na Nje ya Pub. Fanya Pasaka yako iwe safi na Kiluvya Pub.

Advertisements