MAISHA INJE YA BONGO NA KP

Kila kona ya mitaa ya Uingereza katika majiji yote na vitown vidogo kuna bar au Pub, Mitaa imepangiliwa na mtiririko wa nyumba kufuatana, pia mitaa iko safi na mazingira yamepangiliwa pamoja na ujenzi.
Hapo wanafunzi wa chekechea wakitoka shule na wasimamizi wao wakielekea majumbani kwao wakiwa na Hi-vest kwa ajili ya usalama barabarani.

Menus za baa na pabs kama inavyoonekana ratiba ya yaliyomo kwa wiki-end au siku za juma katika pab husika ndani ya Normanton Road Derbyshire Uingereza.

Kituo kidogo cha mabasi (Local transport), hapo sawa na kusubiri basi kutoka Africa-sana kuelekea Kariakoo au Posta Bongo, hapa ni Uingereza nje ya Jiji la London.

Hapa ni Uholanzi, Mitaa yake haitofautiani na Uingereza na ujenzi ukiangalia kwa makini unafanana, Bibi Shirley akiwa na rafiki yake, wabongo waishio Uholanzi.

Advertisements

EASTER HOLLS/PASAKA NDANI YA KP

Sikukuu ya Pasaka [Easter] Husherehekewa Ulimwenguni kote. Kama kawaida Kituo cha Starehe kwa Watu Makini cha Kiluvya Pub mambo kweli yalikuwa mambo. Burudani ya nguvu iliyoweka kumbukumbu Mioyoni mwa waliokuwepo ni ngumu kuisimulia.
Ngoja walao kwa Muhtasari tu uone kupitia Picha. Cha muhimu fanya hima na wewe kama hujawahi kufika Fika hasa siku za Week End nakuhakikishia utafurahia tuu. Karibu sana.

Studio ya Kiluvya Pub.

DJ Muddy. DJ mkali na hatari sana katika miondoko yote Bongo flava mpaka vitu vya mamtoni, akiwalusha Kiluvya Pub mpaka kuchee, Mablaza Men na Masista Duu wanamjua, Viti havikaliki. Jamaa mkali sana.

Ukishajiburudisha namna hii fikra na akili nazo zinatulizana unaporudi darasani kushika kitabu Material yanakubali kiulaini

Hapa kama sikosei nadhani wimbo uliokuwa unachezwa ni Kitambaa cheupe wa King Kikii. Si unaona huyo alivyonyanyua Kitambaa chake cheupe.

Sio lazima uende Dancing Floor. Hapohapo ulipo unaweza kuserebuka mpaka bas.

Heti mzee wa Macharanga Charles Hillary hebu niambie vipi Ile Thatched House ya kule East London inaona ndani kwa Kiluvya Pub?
Swali hilo pia ni kwa Brother Solomon Mugera pia Hassan Mhelella

WIDE SCREEN LIVE FOOTBALL

Hujutii  muda wako unapokuwepo Kiluvya Pub kwani ni mahali ambapo mbali na Burudani kadhaa utajionea Michezo ya Ligi mbalimbali za Barani Ulaya na Afrika pia Mashindano ya Champions League. Huonyeshwa kupitia Screen kubwa kama inavyoonekana hapo. Mashindano ya Kombe la Dunia Yataonyeshwa pia kaa mkao wa kula.

Kiluvya Pub ni Mahali ambako Ligi mbalimbali Barani Ulaya pia Champions League zinaonyeshwa kupiti Screen kubwa kama inavyoonekana hapo katika mpambano baina ya Bayern Munich Vs. Man United

Wapenzi wa Football wanafuatilia Mpambano.

EASTER EASTER EASTER – PASAKA PASAKA PASAKA

EASTER EASTER EASTER – PASAKA PASAKA PASAKA
Usikose uhondo ndani ya Kituo chako cha starehe Kiluvya Pub,
Muziki mkali na Djs waliobobea kutoka Kiluvya Djs Group na Nje ya Pub. Fanya Pasaka yako iwe safi na Kiluvya Pub.

YALIYOJIRI SIKU YA VALENTINES DAY NDANI YA KILUVYA PUB 2010

Binti huyo ndie aliyepata ushindi wa Mnenguaji bora kwa siku hiyo ya Valentine Day. Amepata tuzo ya kitenge cha Wax. hapo anaonesha umahiri wake

Kijana huyo ndie alieonekana na Majaji kuwa ndiye mnenguaji hodari. Hapo anaelekea Dancing Floor kuonesha umahiri wake baada kutangazwa kuwa mshindi kwa upande wa Wanaume. Amepata Zawadi ya Shati zuri sana.

Mshindi wa Valentine Day akionesha na kufurahia zawadi yake ya Simu {Nokia}

Judge akimtangaza mshindi alievaa Ki-Valentine Day ambapo alizawadiwa Simu aina ya NOKIA.

Chief Judge akitangaza Washindi na kueleza vigezo vilivyoyumika kuwapata Washindi hao. Walipatikana wanenguaji hodari wa Kike na Wakiume pia alievaa vizuri Ki-Valentine

Mkuu wa Kitengo cha Itifaki Bwana Lukindo akionesha umahiri katika kucheza Muzidi.

Wahudumu wa Kiluvya Pub wakiwa na Meneja wao Bi. Angel Sanga [Kulia]

Ndani ya Kiluvya Pub Watu wa marika yote wanapata Burudani isiyo kifani inayoporomoshwa na Ma Dj makini kwa Mashine za hali ya Juu. Hupotezi muda wako unapofika Pub. Usingoje kusoma ama kuhadithiwa. Fika mwenyewe uburudike.

Sherehe Ndani ya Ukumbi wa Kiluvya Pub siku ya Wapendanao [Valentine Day]. Wahudumu wakiwa Tayari kutoa Huduma safi isiyo na kasoro ya aina yoyote. Siku hiyo ilikuwa murua sana. Wote waliokuwepo wamesema hawataisahau kwa jinsi walivyostareheka kwa namna mbalimbali.

Vitu vikali ndani ya Pub, Kiluvya Pub Bwana, Wee Acha tuu

Nahisi Wadau Bakari Msulwa huko Tokyo Japan, Joe Nyingo huko Washington DC, Ismail Misigalo huko Kigali Rwanda, Lubunga Biaombe, huko Kinshasa na hata Chekuse Kawawa huko Dublin , Ireland. Mnai Miss Kiluvya Pub!! Au?

BLU 3 feat. MOSES – WHERE YOU ARE, VALENTINES DAY 2010

VALENTINES GIFT!!!!!!!!!!! Fine future tune itafanya Valentine yako iwe swafi, maandalizi makali ndani ya Tarehe 14 Feb hii Djs wakali watafanya Valentine iwe siku ya ndoto kamilifu kati yako na mwenza wako, Usizubae jiandae kuifurahia siku hii muhimu kwa wapendanao ndani ya Kiluvya Pub. Red Roses and white and Red Dress zitatawala na zawadi zitatolewa kwa washindi wa vazi la Valentine. Check it Out in our contacts (About Us) for more details and any doubts

Vodpod videos no longer available.

 

TUTAKUKUMBUKA DAIMA “SIMBA WA VITA”

Msiba wa Taifa, taifa letu tumekumbwa na msiba wa mtu muhimu sana katika Taifa hili hasa ukiangalia historia ya Tanzania kwa undani zaidi. Mzee Rashid Kawawa amefariki katika Hospitali ya rufaa ya Muhimbili na mwili wake kuhifadhiwa katika hospitali ya jeshi ya Lugalo kwa ajili ya mazishi ambayo yamefanyika jana jumamosi nyumbani kwake Madale. 

Atakumbukwa sana kwa mchango wake mkubwa kwa Taifa hili la Tanzania, Mzee Rashid alikuwa Waziri mkuu wa kwanza nchini Tanzania na pia kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi na Makamo wa raisi.  Mzee Kawawa alizaliwa mnamo mwaka 1926 kijijini Matepwende, Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Tanzania. Alihitimu elimu ya msingi mwaka 1942 na kuendelea na elimu ya Sekondari katika shule ya Dar Es salaam sekondary School. 

Mzee Rashid Mfaume Kawawa akiwa na Raisi Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe za Uhuru miaka 48 siku chache kabla ya kifo.

Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali pema peponi. AMINA

Vodpod videos no longer available.

  

Advertisements